Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul_Bayt (a.s) - ABNA - Kufuatia mashambulizi ya utawala haram wa Kizayuni katika maeneo mbalimbali ya Gaza, kuzingirwa kwa ukanda huu, na kufungwa kwa sehemu kubwa ya vivuko hivyo, Wapalestina wanakabiliwa na tatizo la kupata mikate na chakula katika maeneo hayo kiasi kwamba mamia ya Wapalestina katika Mji wa Deir al-Balah, wanakusanyika katika foleni ndefu ili waweze kununua Mkate kutoka katika kiwanda pekee cha kuoka mikate kinachofanya kazi katika eneo hilo, na wanapata shida kubwa katika hilo.